Loading...
Msanii wa Bongo Fleva, Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Palestina iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu na mwili wake umehifadhiwa katika Hospital ya Mwananyamala.
Taarifa hiyo imethibitishwa na msambazaji wa nyimbo zake ambaye pia Meneja wa ‘Team Mtaa kwa Mtaa’, Amri the Business aliyeeleza kwa masikitiko alivyopokea makubwa kuwa Sam amefariki dunia na kumtakia kupumzika kwa amani.
“Siamini kilichotokea muda huu ila sina jinsi, kwani woote safari ni moja, pumzika kwa amani Sam wa Ukweli, hakika nilikupenda kama ndugu yangu wakuzaliwa tumbo moja, #rip” amesema Amri the Business.
Aidha, aliyekuwa mtayarishaji wa nyimbo za Sam wa Ukweli, Producer Steve amesema Sam alizidiwa zaidi Jumamosi iliyopita na walipomuuliza alisema ni ‘UKIMWI wa kulogwa’.
Na Neema Bushubo.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

SAM WA UKWELI AAGA DUNIA, ALIDAI ALIKUWA AKISUMBULIWA NA 'UKIMWI WA KULOGWA'
Reviewed by By News Reporter
on
6/07/2018 11:09:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: