Loading...
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda jana ametangaza kuanza kwa oparesheni kabambe ya kuwakamata na kuwatoza faini wachafuzi wa Mazingira kuanzia July Mosi kwa lengo la kuhakikisha jiji linakuwa kwenye Hali ya usafi kama majiji mengine ulimwenguni.
RC Makonda amesema ameandaa vijana zaidi ya 4,000 kutoka Jeshi la kujenga Taifa JKT ambao watafanya kazi ya kuwakamata watupaji wa taka barabarani na mitaani.
Vijana hao 4,000 ni wale waliomaliza mafunzo ya JKT na hawana kazi ambapo RC Makonda ameamua kuwachukuwa kwaajili ya kufanya kazi hiyo na kwenye kiasi cha faini watakazo watoza wachafuzi wa mazingira 40% itaenda kwa vijana hao na 60% itaingizwa serikalini.
Aidha RC Makonda amesema hawezi kukubali kuona jiji linakuwa kwenye hali ya uchafu wakati ipo sheria ya mwaka 2004 inayotoa mamlaka ya kuwawajibisha wananchi wenye tabia kuchafua mazingira kwa makusudi.
Na Fatma Pembe.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

RC MAKONDA KUWASHIKISHA ADABU WACHAFUZI WA MAZINGIRA
Reviewed by By News Reporter
on
6/06/2018 08:59:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: