Loading...

ROSE NDAUKA AKUMBANA NA SKENDO YA UTAPELI

Loading...
Muigizaji wa Bongo movie Rose Ndauka amepatwa na skendo nzito ya utapeli ambapo amedaiwa kumtapeli mfanyakazi wake kiasi cha shilingi laki na nusu.

Kipindi cha Shilawadu cha Clouds Fm wanaripoti kuwa mwanadada aliyejitambulisha kwa jina la Stumai amemtuhumu Rose kwa kumdhulumu kiasi hicho cha pesa baada ya kumpa huduma.

Kwenye Interview na kituo hicho mwanadada huyo anafunguka kuwa aliajiriwa Kwenye moja ya saluni za Rose Ndauka lakini baada ya kufanya kazi kwa miezi mitatu alikataa kumlipa na kudai hajaona faida hivyo avumilie atakuja kumsaidia kuwa supastaa.

Baada ya povu hilo Soudy Brown alimtafuta Ndauka ambaye alimwaga povu zito kwani hakufurahishwa na taarifa na kumtolea maneno haya:

"Kama kesi inahusu wafanyakazi nenda Kwenye wizara ya Ajira na wafanyakazi sio Shilawadu, Soudy wewe ni mshkaji wangu Sitaki kupizana Kelele na wewe nina stress nyingine za maisha za Familia lakini stress nyingine za kujiunga za kipumbavu kama hizo sitaki kuziongelea kabisa".

Mwishowe Rose amemtaka dada huyo aende mahakamani akashtaki au anaweza akaenda alipokuwa anafanya kazi Mwanzoni.
Na Neema Bushubo.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
ROSE NDAUKA AKUMBANA NA SKENDO YA UTAPELI ROSE NDAUKA AKUMBANA NA SKENDO YA UTAPELI Reviewed by By News Reporter on 6/07/2018 01:16:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.