Loading...

SAMAKI MKUBWA ZAIDI DUNIANI APATIKANA MAFIA

Loading...
Je unamjua Papa Potwe? (Whale Shark) ni Samaki mkubwa duniani na huweza kufikia hadi mita 18. Akiwa mdogo huwa na kimo cha basi dogo la abiria.

Samaki hawa hupatikana maeneo machache duniani, na kwa mujibu wa watafiti wa bahari ni miongoni mwa viumbe vilivyopo hatarini kutoweka.

Moja ya maeneo wanayopatikana ni kisiwani Mafia Tanzania, sehemu nyingine ni kama Mexico na Philipenes.

Kutokana na umuhimu wa samaki huyu wavuvi pamoja na wahifadhi wa bahari wamekua na jitihada za kuwalinda viumbe hawa.

Katika maeneo ya ufukwe wa Mafia mjini, naambiwa kuwa samaki hawa wakubwa duniani ikifika msimu wake basi huonekana hata ukiwa ufukweni, huna haja ya kuingia baharini labda tu ukitaka kuogelea nao.

Papa Potwe hujulikana pia kama Papa mwema kwa ukarimu wake, hufuata wavuvi na watalii wakiwa ndani ya maji na hucheza nao.

Kwa kipindi cha mwaka mmoja Papa Potwe huweza kusafiri hadi kilomita 10,000.Lakini watafiti wanasema kuwa Papa Potwe wa kisiwani mafia hubaki eneo moja kwa muda mrefu.

Mbali na jitihada zinazofanyika lakini bado Samaki hawa wanakumbwa na hatari kubwa kutokana na shughuli za uvuvi., na kama jitihada za ziada zisipofanyika basi itabaki historia kuwa kulikuwa na Samaki wakubwa duniani.
Na Catherine Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
SAMAKI MKUBWA ZAIDI DUNIANI APATIKANA MAFIA SAMAKI MKUBWA ZAIDI DUNIANI APATIKANA MAFIA Reviewed by By News Reporter on 6/01/2018 08:03:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.