Loading...

TRUMP ASUBIRI BARUA KUTOKA KWA KIM JONG UN

Loading...
Rais Donald Trump amesema kuwa anatarajia barua kutoka kwa rais wa Korea Kaskazini kumfikia hivi karibuni.

Hii ni baada ya generali wa ngazi ya juu wa Korea Kaskazini kufanya mkutano na waziri wa mambo ya nje wa Marekani mjini New York.

Mazungumzo kati ya viongozi hao wawili yameonekana kuzaa matunda kwani Trump anatarajia kuwa yeye na Kim wanaweza kukutana 12 Juni nchini Singapore.

Hata hivyo Trump amewaambia waandishi wa habari wakati akiwa katika uwanja wa ndege wa Maryland kuwa hadhani kama maafikiano yatafikiwa katika kutano mmoja.

"Nadhani tunaweza kukutana zaidi ya mara moja",alisema Trump.

Marekani vilevile imesisitiza kuwa mkutano huo utakuwa na maana pale tu Korea Kaskazini itakapofanya maamuzi ya kuachana na silaha za nyuklia.

Hapo awali Kim alisema kuwa Korea Kaskazini itaachana an makombora hayo lakini kwa muda inayotaka yenyewe.
Na Geofrey Okechi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
TRUMP ASUBIRI BARUA KUTOKA KWA KIM JONG UN TRUMP ASUBIRI BARUA KUTOKA KWA KIM JONG UN Reviewed by By News Reporter on 6/01/2018 10:21:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.