Loading...

ASLAY ADAI UONGO WA WANAWAKE UMESABABISHA KUYACHUKIA MAPENZI

Loading...
Staa wa Muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake ya 'Totoa' Aslay Isihaka amefunguka na kuweka wazi kuwa hana Mpango wa kuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi kwa sasa.

Aslay ambaye mwezi uliopita alitangaza kuachana na aliyekuwa mpenzi wake na mama watoto wake Tessy Chocolate bila kuweka wazi sababu ya wawili hao kuachana.

Tangu Aslay  ameachana na Tessy amedaiwa kuwa kimapenzi na Muigizaji Diana Kimary jambo ambalo hata yeye alithibitisha Lakini hivi sasa Msanii huyo anafai hayataki Tena mapenzi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari Aslay amefunguka na kuweka wazi kuwa kwa saaa hajali kuhusu kuwa na mwanamke kwani wengi wao ni waongo wanaangalia pesa tu:

"Katika vitu ambavyo Sivipi kipaumbele kwa sasa ni Mahusiano na wanawake maana wengi wao hawana mapenzi ya kweli, hawajali maisha ya mtu au hawaamini kuwa fulani amepata leo pesa au amekosa".

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa Aslay amerudiana na aliyekuwa mpenzi wake Amber Lulu taarifa ambazo Aslay amezikataa na kusisitiza kuwa hana mpenzi kwa sasa na wala hahitaji.
Na Hamisi Fakhi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
ASLAY ADAI UONGO WA WANAWAKE UMESABABISHA KUYACHUKIA MAPENZI ASLAY ADAI UONGO WA WANAWAKE UMESABABISHA KUYACHUKIA MAPENZI Reviewed by By News Reporter on 7/19/2018 05:04:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.