Loading...
Hifadhi moja ya kutengeneza iliyopo nchini Misri, mji mkuu wa Cairo, imekataa shutuma za kumpaka rangi farasi kwa madai kuwa ni Pundamilia.
Hebu angalia picha hiyo juu na kisha fanya uchunguzi na jaji mwenyewe.
Picha hiyo ilipigwa na kijana mwenye umri wa miaka 18 kwa jina alitambulika kama Mahmoud Sarhan katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Gardens Park huko Cairo na ilisambazwa zaidi ya mara 7,500 kupitia kurasa za mtandao wa Facebook.
"Tumemaliza utalii wetu na tuliamua kupiga baadhi ya picha... Wakati pundamilia alipokuja karibu na mimi, Nilikiri kuwa ni farasi aliyepakwa rangi za pundamilia," Mahmoud alinukuliwa Katika gazeti moja la UK la Metro.
Na hii kwa sasa inaonekana kuwa hali ya kawaida, mnamo mwaka 2009, hifadhi moja huko Gaza iliwachora pia farasi wawili ili kuziba pengo la pundamilia waliofariki kwa njaa kipindi cha vita.
Udanganyifu unaofanyika kwa sasa umeanza kuwachosha watalii katika hifadhi za kutengeneza kukosa hamasa za kutembelea hifadhi hizo.
Na Neema Joshua.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

HIFADHI YASHUTUMIWA KUMPAKA RANGI FARASI ILI AONEKANE PUNDAMILIA
Reviewed by By News Reporter
on
7/28/2018 09:16:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: