Loading...

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA RONALDO BAADA YA KUONDOKA REAL MADRID

Loading...
Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno anayeichezea club ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo baada ya headlines za muda mrefu na kuhusishwa kujiunga na club ya Juventus ya Italia leo hatimae amejiiunha rasmi na club hiyo.

Ronaldo amejiunga na Juventus kwa mkataba wa miaka minne ambao utamuweka katika club hiyo hadi mwaka 2022, Juventus wamekubaliana na Real Madrid kumnunua Ronaldo kwa dau la euro milioni 100 ambapo itaongezeka euro milioni 12 itakayolipwa katika kipindi cha miaka miwili.

Ronaldo baada ya kuondoka Real Madrid ametoa ujumbe wa wazi kwa mashabiki, uongozi wa Real Madrid na kuwashukuru kwa kipindi chote cha miaka tisa ambacho kimekuwa kwa mafanikio makubwa kwake, kwa kufanikiwa kushinda Ballon d’Or mara nne na Champions League mara 4.
“Kwa miaka yote hii nikicheza Real Madrid na nikiishi katika mji wa Madrid umekuwa ni wakati wa furaha katika maisha yangu, kwa mapenzi makubwa naomba niishukuru hii club nawashukuru wote kwa kwa mapenzi makubwa walionionesha,” aliandika Ronaldo.

“Kiukweli nimekuwa na miaka tisa ya furaha na mafanikio, imekuwa ni miaka tisa ya kipekee, nafahamu vizuri kuwa sitaweza kusahau kipindi changu cha furaha Real Madrid kikiwa cha kipekee,” aliongeza CR7.
Na Neema Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
HIKI NDICHO ALICHOKISEMA RONALDO BAADA YA KUONDOKA REAL MADRID HIKI NDICHO ALICHOKISEMA RONALDO BAADA YA KUONDOKA REAL MADRID Reviewed by By News Reporter on 7/11/2018 10:30:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.