Loading...
Mwanamuziki maarufu kutoka Canada Justin Bieber amemposa mwanamitindo nchini Marekani Hailey Baldwin, vyombo vya habari vinaripoti Marekani.
Hailey Baldwin ni mwanamitindo mwenye umri wa miaka 21 tu, anafahamika zaidi huko Marekani baada ya kutokea katika televisheni mbali mbali.
Hailey ni mtoto wa mwigizaji wa kimarekani Stephen Baldwin na mama yake ni mbrazil Kennya Deadato Baldwin.
Hata hivyo ana undugu na mwigizaji maarufu duniani Alec Baldwin ambaye ni baba yake mdogo.
Amewahi kutokea katika majarida mbali mbali kama vile Vogue, Talter, LOVE, na I-D.
Pia Hailey ni mwanamitindo aliye pita katika matamasha mbali mbali ya mitindo kama vile Pre-London fashion week, Millan fashion week na New York fashion week. Huku akitokea katika matangazo ya televisheni ya H&M, TommyHilfiger na mengine mengi.
Hailey pia ametokea kwenye video za muziki kama vile On my Mind ya Cody Simpson na video ya love to love you.
Pia ametangaza katika matamasha ya iHeart Radio mwaka 2016 na MTV Europe mwaka 2016.
Na amekuwa na marafiki wengi wa karibu ambao ni maarufu kama vile wana mitindo Gigi na Bella Hadid, Kendal na kylie Jenner.
Kitaaluma Hailey Baldwin alikuwa na malengo ya kuwa dansa wa mtindo wa Classic Ballet, lakini aliacha baada ya kupata jeraha mguuni.
Hailey na Justine Bieber waliwahi kuwa na mahusiano mwaka 2015 kipindi ambacho Justine alikuwa ameachana na Selena Gomez.
Wamerudiana tena mwezi may mwaka 2018 baada ya Justine kuachana na Selena Gomez kwa mara nyingine Tena.
Hailey amevalishwa pete ya uchumba na Justine Bieber mwenye umri wa miaka 24 katika hoteli ya kitalii Bahamas. Kwamujibu wa TMZ walinzi wake waliwataka watu wote waliokuwa katika mgahawa huo kuweka mbali simu zao kabla Justine haja mvisha pete Hailey.
CNN pamoja na E! wamethibitisha taarifa hizo ambapo wazazi wa Bieber pia walithibitisha kwa kuonyesha furaha zao kupitia mitandao yao ya kijamii.
Baba yake Justine, Jeremy Bieber aliweka picha ya mtoto wake katika mtandao wa Instagram na kuandika kuwa anafurahia ukurasa unao fwata. Huku mama yake Justine akiandika kupitia ukurasa wake wa Twiter LOVE LOVE
Mwanadada huyu Kait ameandika, 'iwapo ni kweli Justin Bieber amemchumbia Hailey Baldwin. Moyo wangu umevunjika mara mbili, moja kwa ajili yangu na pili kwa ajili ya Selena'.
Kabla ya kurudiana na Justine Bieber mwaka huu Hailey Baldwin kupitia mitandao ya kijamii alitajwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki Shawn Mendes baada ya kuhudhuria tamasha la Met Gala kwa pamoja. Hata hivyo kupitia vyombo mbalimbali vya habari shawn mendes alikanusha taarifa hizo na kusema kuwa wao sio wapenzi.
Na Neema Bushubo.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

JE UNAMJUA MSICHANA ALIYEVISHWA PETE NA JUSTIN BIEBER?
Reviewed by By News Reporter
on
7/10/2018 05:57:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: