Loading...

JIKO LA KISASA LINALOTUMIA MAJI NA MAFUTA MACHAFU, LAGUNDULIWA SABASABA

Loading...
Wafumbuzi na wabunifu wa Tanzania wamekuja na teknolojia mpya ya kutunza mazingira.

Teknolojia hiyo itasaidia pia kupunguza gharama za nishati kwa kiasi kikubwa.

Teknolojia hiyo kwa mara ya kwanza imeonekana katika banda la Mali asili na Utalii maonesho ya kimataifa ya 42 ya sabasaba jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti mkuu wa utanzaji mazingira wa Karatu Aloyce Songay aliliambia gazeti moja la hapa nchini kwamba Wilaya yao inakabiliwa na changamoto ya utunzaji wa mazingira kwa kuwa wanatumia sana kuni kama nishati ya kupikia.

"Tumekuja na bunifu nyingi sana kama kuunda aina mbili za majiko yanayotumia kuni na baadae kutengeneza majiko ya kupikia yanayotumia mafuta machafu na maji.

Ni nafuu na safi. Linatumia lita 10 ya mafuta machafu kwa Sh4,000 na lita 2 za maji kwa kila mwezi," alisema

Jiko hilo linauzwa kwa thamani ya Sh500,000.

Alidokezea kwa kusema jiko hilo lina bomba la kutolea moshi wakati wa kupikia kwahiyo ni safi na salama.
Na Fatma Pembe.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
JIKO LA KISASA LINALOTUMIA MAJI NA MAFUTA MACHAFU, LAGUNDULIWA SABASABA JIKO LA KISASA LINALOTUMIA MAJI NA MAFUTA MACHAFU, LAGUNDULIWA SABASABA Reviewed by By News Reporter on 7/09/2018 04:10:00 PM Rating: 5

Maoni 1 :

  1. Ubunifu na ugunduzi wa msingi na wa hali ya juu, mimi nipo interested

    JibuFuta

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.