Loading...

UTAFITI: HUENDA ULAJI WA UGALI, NYAMA NA MAZIWA UNATUUA KIMYA KIMYA

Loading...
Huenda watu waishio Afrika Mashariki wanahatarisha maisha yao kutokana na unywaji kwa wingi wa maziwa, ulaji nyama na vyakula vya nafaka vinavyosemekana viko na sumu ya aflatoxin ambayo imepita kiwango kinachokubaliwa na shirika la Agricultural Organisation (FAO).

Kulingana na utafiti, vyakula vinavyotokana na wanyama ambavyo vinanunuliwa madukani vina kiwango kikubwa cha sumu ya aflatoxin hivyo basi ni hatari kwa afya ya binadamu. 

"Watu wengi wanakula vyakula ambavyo viko na kiwango cha juu cha sumu ya aflatoxin huku wakihatarisha maisha yao ilhali nchi zimekuwa katika mstari wa mbele kupiga vita dhidi ya magonjwa kama saratani," mtafiti Johana Lindahl wa nchini Kenya alisema.

Utafiti huo pia ulionyesha kwamba asilimia 72% ya maziwa ya ng'ombe 84% kutoka kwa wakulima wa juu na wa kati na asilimia 99% ya maziwa ya pakiti yako na sumu hiyo ya aflatoxin.

Unga wa ugali unaotumiwa na watu wengi katika nchi hizi pia uko na hatari zake kulingana na utafiti huo. " Sumu ya aflatoxin iko kwa wingi sana hasa kwenye mahindi na wakulima na wafanya biashara wanapaswa kuelimishwa kuhusiana na hatari za sumu hii na wapatiwe namna za kuzuia milipuko ya maradhi yoyote," Lindahl aliongezea.

Utafiti huu unatokea huku kukiwa na wasiwasi baina ya nchi zetu kuhusiana na sukari haramu inayosemekana kuwa na madini ya zebaki na shaba na ambayo ni hatari kwa matumizi ya binadamu.
Na Hamisi Fakhi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
UTAFITI: HUENDA ULAJI WA UGALI, NYAMA NA MAZIWA UNATUUA KIMYA KIMYA UTAFITI: HUENDA ULAJI WA UGALI, NYAMA NA MAZIWA UNATUUA KIMYA KIMYA Reviewed by By News Reporter on 7/09/2018 04:56:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.