Loading...

MAANDAMANO YASIMAMISHA MRADI WA UCHIMBAJI WA MAFUTA - KENYA

Loading...
Kampuni ya kuchimba mafuta ya Tullow imesitisha operesheni zake Turkana kwa sababu ya maandamano yaliyojawa na fujo na ongezeko la ukosefu wa usalama eneo hilo.

Uamuzi huo ulifanywa mwezi mmoja baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuzindua usafirishaji wa mafuta kutoka Ngamia 8 hadi bandarini Mombasa.

Katika taarifa iliyoonekana na mtandao mmoja wa habari huko Kenya Jumatano, Julai 25, kampuni hiyo ilisema maandamano hayo yamefanya ugumu wa kuendelea kwa operesheni za kazi.

"Wakazi wanatumia usafirishaji wa mafuta kulalamikia serikali ya kitaifa, lazima hali ya usalama iimarike," alisema mkurugenzi wa Tullow, Paul McDadde.

Mkurugenzi hata hivyo alisema kazi itaendelea endapo hali ya usalama itaimarika, "Tutaendelea na operesheni za kikazi hali ya usalama ikiimarika na serikali ikikabiliana na changamoto zilizopo," alisema mkurugenzi huyo.

Siku kadhaa zilizopita, Tullow ilifunga visima vya maji safi kwa sababu ya maandamano.
Mnamo Julai 16, kampuni hiyo pia ilisitisha huduma zake zote kwa jamii na kutishia kuwafuta kazi wakazi wa eneo hilo kwa sababu ya maandamano.
Na Hamisi Fakhi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MAANDAMANO YASIMAMISHA MRADI WA UCHIMBAJI WA MAFUTA - KENYA MAANDAMANO YASIMAMISHA MRADI WA UCHIMBAJI WA MAFUTA - KENYA Reviewed by By News Reporter on 7/26/2018 10:21:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.