Loading...
Vita dhidi ya uuzaji wa pombe haramu katika kaunti ya Taita Taveta vinazidi kupata changamoto huku wagema wa pombe hiyo haramu wakiwatishia polisi kwa uchawi.
Kwa mujibu wa naibu kamishna eneo la Mwatate, Kenneth Muriungi, watu wengi wa eneo hilo wanaamini sana mambo ya uchawi na hivyo kuleta changamoto vita dhidi ya pombe haramu.
"Kuna imani za kushangaza kwa uchawi katika kaunti hii ndogo, hasa katika kata ya Saghaighu. Eneo hilo litakuwa na naibu chifu hivi karibuni kukabiliana na hali hiyo," Alisema kwa mujibu wa The Standard siku ya Jumatano, Julai 25.
Alikariri kuwa licha ya changamoto za uchawi, wagema 300 wa pombe hiyo haramu wamekamatwa na lita 20,000 za pombe hiyo zikinaswa.
Pia, alisema kuwa maafisa wa utawala waliokuwa wakiendesha zoezi hilo la kuwasaka wagema hao litaendelea licha ya vitisho.
Na Neema Joshua.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

WAUZAJI WA POMBE HARAMU WATUMIA UCHAWI KUWAFUKUZA POLISI
Reviewed by By News Reporter
on
7/27/2018 09:52:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: