Loading...
Mume na mke wamejikuta wakitafunwa na ndumba za mganga baada ya kutaka utajiri kwa njia za kishirikina.
Katika kijiji cha Mitaboni kaunti ya Machakos huku Kenya, ndugu, jamaa na marafiki wanaomboleza kifo cha mume na mke.
Wawili hao inaaminika wamefariki dunia baada ya ndumba za kuimarisha biashara yao ili wawe matajiri zilipofeli kutoa matokeo walioyatarajia.
Kulingana na mdokezi, wawili hao walikuwa wametoka mjini Mombasa kumwona mganga ili kupewa hirizi za kuboresha biashara yao ila madawa yaliwageukia.
Wiki moja tu baada ya kufika kutoka Mombasa, mtoto wao alifariki kwa njia isiyo ya kueleweka, ambayo wenyeji walidai kuwa inawezekana kuwa wawili hao walimtoa kama kafara.
Siku chache baadaye, wenyeji walishangaa kuwapata wote wamefariki.
Iliwalazimu wahubiri na wenyeji kuandaa maombi ili kuikomesha mizimu isije ikawaandama waliosalia katika familia hiyo.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

KISA CHA AJABU: WATAFUNWA NA NDUMBA ZA MGANGA KISA UTAJIRI
Reviewed by By News Reporter
on
7/27/2018 02:40:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: