Loading...

DIAMOND AKIRI KUZUILIWA JK NYERERE AIRPORT NA BASATA

Loading...
Mwanamuziki Diamond Platnumz amesema alilazimika kusubiri kwa saa tisa ili kuendelea na safari baada ya kuzuiwa katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa kutokuwa na kibali cha Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) cha kufanya onyesho nje ya nchi.

Mwanamuziki jana huyo alikuwa akielekea katika visiwa vya Madagascar na Mayote ambako atatumbuiza leo (Julai 27) na kesho (Julai 28).

Meneja wa mwanamuziki huyo, Babu Tale amesema Diamond alitakiwa kuondoka jana Saa 3.00 asubuhi lakini baada ya kuzuiliwa ilibidi aondoke saa 11.00 jioni baada ya kukamilisha taratibu za kupata kibali hicho.

“Ni kweli jana msanii wangu (Diamond) alikumbana na mkono wa Basata akiwa uwanja wa ndege. Kwa kuwa tulishalipwa hela ya watu ikabidi tukishughulikie kibali haraka ili aweze kuondoka nchini,” anasema.

Hata hivyo, alilaumu Basata kwa kushindwa kuweka wazi kanuni zake ili wasanii wazijue badala ya kuwasubiri wakosee ili wawachukulie hatua.

“Ninashauri kama Basata wana chochote wanataka wasanii wakifanye wakishirikishe ili kuepusha mzozo,” anasema.
Na Catherine Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
DIAMOND AKIRI KUZUILIWA JK NYERERE AIRPORT NA BASATA DIAMOND AKIRI KUZUILIWA JK NYERERE AIRPORT NA BASATA Reviewed by By News Reporter on 7/27/2018 02:52:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.