Loading...

MAPACHA WALIOUNGANA WALAZWA ICU BUGANDO

Loading...
Watoto pacha waliozaliwa wakiwa wameungana wamelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya  Rufaa ya Bugando.

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo leo Julai 27 Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Dk Abel Makubi amesema watoto hao wa kiume walizaliwa kwa njia ya upasuaji na wataalamu wa afya wameona wanahitaji uangalizi maalumu.

Dk  Makubi alikuwa akimtembeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella aliyekwenda kuwaona pacha hao.

Kwa mujibu wa Dk Makubi watoto hao wamezaliwa na Angelina Ramadhani (34) mkazi wa Nyakato jijini Mwanza, wameungana sehemu ya kifua na tumbo.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo mama wa watoto hao anaendelea vizuri.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema kulingana na taratibu za kitabibu haikuwezekana kuwaona watoto hao badala yake taarifa zitakuwa zikitolewa na wataalamu kulingana na maendeleo yao.

“Niombe tu, kuna taarifa zimeshasambazwa kwenye mitandao ambazo zinapotosha jambo hili, watoto nimewaona kwa macho wanaendelea vizuri hata mimi nilidhani tungeweza kuwaona sote lakini kila kitu kina miiko na taratibu zake,” amesema Mongella.
Na Hamisi Fakhi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MAPACHA WALIOUNGANA WALAZWA ICU BUGANDO MAPACHA WALIOUNGANA WALAZWA ICU BUGANDO Reviewed by By News Reporter on 7/27/2018 02:59:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.