Loading...
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema amefagilia utendaji kazi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola akibainisha kuwa ameanza na kasi nzuri.
Amesema Lugola akiendelea na kasi hiyo ataweza kuvaa viatu vyake alipokuwa waziri wa wizara hiyo wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Pili.
Mwenyekiti huyo wa bodi ya Taifa ya Parole na mbunge wa zamani wa Vunjo ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Julai 27, 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini hapa.
“Lugola ameanza vizuri amenifurahisha pale aliposema kuwa atahakikisha anadhibiti watu kubambikiziwa kesi na baadhi ya askari wasio waaminifu,"amesema Mrema.
Amesema wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, watu walimchukia kutokana na utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na kuwakamata watumishi wa Serikali waliokiuka utaratibu na kufanya makosa.
“Nilisema wizara zote zangu na aliyefanya kosa alikamatwa. Nilikuwa kero kwa baadhi ya watu, lakini sikujali na hicho ndio anakifanya Lugola kwa sasa, nampongeza kwa hilo,” amesema.
Amesema yupo tayari kumwonyesha Lugola kile alichokiita vichochoro alivyovipitia katika utendaji kazi wake wa wakati huo ili vimsaidie waziri huyo katika utekelezaji wa majukumu yake.
Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

MREMA AMPA DOLE GUMBA LUGOLA, ASEMA ANAWEZA KUVAA VIATU VYAKE
Reviewed by By News Reporter
on
7/27/2018 03:15:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: