Loading...

MAGEREZA WATOA MSAADA WA KISHERIA KWA WAFUNGWA MKOANI TABORA

Loading...
Magereza mkoani Tabora imeweka maafisa wake ambao ni wanasheria katika magereza sita yaliyoko mkoani humo.

Uamuzi huo umelenga kuhakikisha wafungwa na mahabusu walioko katika magereza hayo wanapata msaada wa kisheria na hivyo kutekeleza kwa vitendo haki jinai.

Mkuu wa Magereza mkoani Tabora Mratibu Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Hamza Rajabu Hamza ameiambia timu ya wataalamu wa jukwaa la haki jinai iliyopo mkoani Tabora inayotembelea Magereza na vituo vya Polisi mkoani humo na kuzungumza na wafungwa na mahabusu.

Ameyataja magereza hayo kuwa ni Gereza Kuu Uyui, Gereza la Kilimo Urambo, Gereza la Mahabusu Tabora, Gereza Mahabusu Urambo, gereza la Nzega na Gereza la Igunga.

Timu ya wataalamu kutoka Jukwaa la Haki Jinai nchini ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome inatembelea Magereza na vituo vya polisi katika mikoa ya Singida,Tabora, Geita, Kigoma, Mwanza na Kagera ili kujionea changamotozinazowakabili wafungwa na mahabusu katika mikoa hiyo ili kupata hakijinai wanapokuwa vizuizini na kuangalia namna ya kuzitatua.

Ziara hiyo ni utekelezaji wa mradi wa upatikanaji haki na ulinzi wa haki za binadamu nchini unaoendeshwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa –UNDP.
Na Neema Joshua.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MAGEREZA WATOA MSAADA WA KISHERIA KWA WAFUNGWA MKOANI TABORA MAGEREZA WATOA MSAADA WA KISHERIA KWA WAFUNGWA MKOANI TABORA Reviewed by By News Reporter on 7/23/2018 09:22:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.