Loading...

'MAXI PRIEST' MSANII MKONGWE WA REGGAE KUDHURU AFRIKA MASHARIKI AGOSTI

Loading...
Ni habari njema kwa wapenda mziki aina ya reggae kwani msanii shupavu wa raga maarufu kama Maxi Priest anakuja Afrika Mashariki, huko Kenya kuwatumbuiza na mziki wake wa reggae. 

Mtandao mmoja wa habari nchini Kenya imethibitisha kuwa msanii huyo atakuja nchini Agosti 12, 2018 na kuwatumbuiza wapenzi wa reggae katika Ngong racecourse Waterfront jijini Nairobi.

Atatumbuiza kwanzia saa sita hadi saa moja jioni na tayari tiketi kwa wale wanaotaka kwenda katika burudani hiyo zishatolewa.

Tiketi inauzwa kwa Sh 1800 pesa za Kenya, kwa wale watakaoinunua na wale watakochelewa kuinunua watainunua kwa Ksh 2500 kwa kila moja. 

Kulingana na habari za mtandao huo, burudani hiyo itakuwa na vinywaji na vyakula na michezo za watoto na watu wa umri wote wamekaribishwa. 

Mwimbaji huyo shupavu ametoa ngoma kadhaa ambazo zitawakumbusha wengi enzi zile wakati mziki ulikua mziki, wakati reggae ilikua reggae.

Baadhi ya ngoma maarufu zitakazochezwa ni pamoja na Close to you, Just a Little Bit Longer, That Girl, If I Gave My Heart to You na Loving You is Easy miongoni mwa nyingine kadhaa. 

Wasanii wengine kutoka Jamaica ambao wamezuru Kenya ni pamoja na Roman Virgo, Glen Washington, Cecile na Alain ambaye amefanya collabo na mwibaji wa nyimbo za injili Willy Paul, wimbo ambao ulichanganya na kuwashangaza wengi.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
'MAXI PRIEST' MSANII MKONGWE WA REGGAE KUDHURU AFRIKA MASHARIKI AGOSTI 'MAXI PRIEST' MSANII MKONGWE WA REGGAE KUDHURU AFRIKA MASHARIKI AGOSTI Reviewed by By News Reporter on 7/12/2018 01:24:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.