Loading...
Tangu zamani vitu mbalimbali hata wanyama vimekuwa vikitumika kutabiri matokeo ya michezo mbalimbali na Kombe la Dunia mwaka huu, mambo sio tofauti.
Lakini utabiri kutumia wanyama sio kitu kipya na kote ulimwenguni, umekuwa ukifanyika tangu zamani sana.
Kwenye michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Urusi, wanyama kama vile kobe, pweza, paka wametumiwa sana na matokeo yakawa kweli ama yakawa sivyo.
Tuangalie mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Dunia kati ya Croatia na England ambapo kobe alitabiri matokeo.
Katika mechi hiyo iliyoishia 2-1, Trippier alifunga bao la kwanza dakika za mwanzo wa kipindi cha kwanza kupitia mpira wa adhabu na kuiweka England almaarufu Three Lions mbele.
Mshambuliaji wa Inter Milan Ivan Perisic aliisawazishia Croatia, na kusababisha mechi hiyo kuingia muda wa ziada.

Utabiri wa kobe ulikuwa umesema kuwa, Croatia wangeshinda mechi hiyo na muda wa ziada ulipojiri mambo yalibadilika huku isijulikane nani angeibuka mshindi.
Muda huo, ulimpa nafasi Mario Mandzukic kufunga bao lililomchanganya golikipa wa England Jordan Pickford na lililowabeba hadi fainali ya Kombe la Dunia na utabiri wa kobe huyo kutimia.
HUYU NDIYE KOBE ALIYETABIRI USHINDI WA CROATIA DHIDI YA UINGEREZA
Reviewed by By News Reporter
on
7/12/2018 11:55:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: