Loading...

MKUTANO WA NATO: TRUMP ATOFAUTIANA NA WENZAKE KUHUSU BAJETI YA ULINZI

Loading...
Rais wa Marekani amewataka viongozi wengine wa nchi wanachama wa Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi NATO kuongeza bajeti ya ulinzi, hali ambayo imezua mvutano kati ya mataifa wanachama wa umoja huo.

Wakati huo huo Rais Donald Trump ameishtumu Ujerumani kwamba inatumia kiasi kidogo, katika bajeti ya ulinzi wakati ambapo inatumia fedha nyingi katika ununuzi wa bidhaa za nishati, kutoka nchini Urusi,taifa ambalo walipa kodi wa Marekani wanachangia kodi zao kukabiliana na vitisho vyake.

Mkutano wa Brussels unakuja ikiwa ni takribani wiki moja tu kabla ya Rais Trump kuwa na mkutano wa kwanza na rais wa Urusi Vladmir Putin mjini mjini Helsinki nchini Finland.

Licha ya rais Trump kuhimiza washirika hao wa NATO kuwa na ongezeko la bajeti ya ulinzi,lakini wanachama wa NATO wamesema hayawezi kutimiza ahadi zao ifikapo mwaka 2024.

Rais Donald Trump amewataka washirika wa NATO kuongeza kiasi cha fedha mara mbili zaidi kwa ajili ya kuongeza bajeti ya ulinzi ambayo kwa sasa wanachangia asilimia mbili tu,na yeye akiwataka kufikia mchango wa asilimia nne kutoka kwenye pato la mataifa hayo.
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MKUTANO WA NATO: TRUMP ATOFAUTIANA NA WENZAKE KUHUSU BAJETI YA ULINZI MKUTANO WA NATO: TRUMP ATOFAUTIANA NA WENZAKE KUHUSU BAJETI YA ULINZI Reviewed by By News Reporter on 7/13/2018 09:11:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.