Loading...

REAL MADRID WAANDAA KITITA CHA EURO 150MIL KUMNYAKUA HAZARD

Loading...
Klabu ya Real Madrid inaandaa kitita cha Euro milioni 150 ili kumnyakua mshambuliaji machachari wa klabu ya Chelsea anayechezea timu ya taifa ya Ubeligiji katika msimu huu wa joto.

Klabu hiyo ya Uhispania imeweka wazi kuwa Hazard ndio malengo yao kwa sasa wanayemsaka kwa hudi na uvumba, baada ya kumuuza Christian Ronaldo kwa Juventus kwa Euro milioni 100.

Mabingwa hao wa Ulaya wanaamini watamnyakua nahodha huyo wa Ubeligiji, ambaye amebakiza miaka miwili kumaliza mkataba wake katika klabu ya Chelsea, ili aelekee Hispania.

Hazard alifunguka wiki hii juu ya 'Upekee' halisi wa jezi ya Real Madrid na jinsi walivyo akidai 'ni klabu ambayo inatimiza ndoto zako'.

Ingawa nyota huyo wa miaka 27, alisema yupo vizuri na klabu yake ya sasa, lakini mara nyingi huwa na ndoto ya kuchezea Bernabeu.

Chelsea hawawezi kuendelea kumg'ang'ania kwa kumlipa euro laki 3 kwa wiki na mwezi uliopita Hazard aliwapa changamoto klabu hiyo kukubali kiasi hicho kabla hawajalipa pesa hizo.

Kwa upepo huo, Hazard mbioni kwenda kurithi mikoba ya CR7.
Na Hamisi Fakhi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
REAL MADRID WAANDAA KITITA CHA EURO 150MIL KUMNYAKUA HAZARD REAL MADRID WAANDAA KITITA CHA EURO 150MIL KUMNYAKUA HAZARD Reviewed by By News Reporter on 7/13/2018 09:45:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.