Loading...

MWANAMUZIKI KOFFI AZUILIWA KUINGIA ZAMBIA

Loading...
Serikali ya Zambia imemuzuia mwanamziki maarufu wa nyimbo za aina ya Rhumba, Koffi Olominde kungia nchini humo kuwatumbuiza wafuasi wake.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 62 na raia wa Congo, alikashifiwa kwa kumshambulia mwanahabari mmoja nchini humo mwaka wa 2012. 

Taarifa za BBC ziliarifu kuwa Olomide pia alishtumiwa kwa kuwanyanyasa kingono wachezaji wake wa densi, kuwateka nyara na kuwaajiri kwa kutumia stakabadhi ghushi.

Akihojiwa na wanahabari wa Zambia, Koffi alijutia kitendo hicho na kuwaomba msamaha wafuasi wake kutoka Zambia. 

Aidha, serikali ya Zambia imeonya kwamba itamtia mbaroni mwanamuziki huyo endapo atajaribu kungia nchini humo kwa nguvu. 

Itakumbukwa kwamba , Koffi alihawahi zuiwa kuwatumbuiza Wakenya mwaka wa 2016 baada ya video kuibuka mitandaoni akimpiga mmoja wa wachezaji wake wa densi.

Kisa hicho kilipelekea serikali ya Kenya kuamrisha Koffi kufurushwa nchini haraka iwezekanavyo na kufutilia mbali tamasha yake ya burudani aliyokuwa ameandaliwa.
Na Haika Gabriel.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MWANAMUZIKI KOFFI AZUILIWA KUINGIA ZAMBIA MWANAMUZIKI KOFFI AZUILIWA KUINGIA ZAMBIA Reviewed by By News Reporter on 7/18/2018 03:48:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.