Loading...

SISTER FEY ATAKA KUMCHAPA PAPARAZI KISA KIBEN 10

Loading...
Msanii wa muziki Sister Fey alizua gumzo baada ya video moja wapo kusambaa akitaka kumpiga vibao mwandishi aliekutana nae buchani akiwa na mpenzi wake baada ya kumhoji maswali yanayohusiana na mahusiano yake hayo mapya.

Hasira ya Sister Fey ilikuja baada ya mwandishi huyo kumuuliza Sister Fey anajisikiaje kuwa katika mahusiano na mtoto mdogo ndipo aliposhikwa na hasira na kumpiga kibao na kukataa tena kufanya nae mahojiano.

Tangu sister fey atangaze na kuweka mitandaoni mahusiano yake mapya, kumekuwa na waandishi wengi wakitaka kujua undani wa penzi hilo hivyo amekuwa akikutana na interviews nyingi sana .

kwa hasira sister fey alisikika akisema “huyo sio mtoto huyu ni mume wangu tena uwe na adabu sawa..pum***** tena uwe na adabu siku nyingine usirudie huyu ni mume wangu.” Alisema Sister Fey kwa hasira na kuondoka eneo la tukio.
Na Paskali Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
SISTER FEY ATAKA KUMCHAPA PAPARAZI KISA KIBEN 10 SISTER FEY ATAKA KUMCHAPA PAPARAZI KISA KIBEN 10 Reviewed by By News Reporter on 7/18/2018 12:21:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.