Loading...

RAIS MAGUFULI AMEIBUKA MSHINDI WA TUZO YA UKOMBOZI WA AFRIKA

Loading...
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ameibuka mshindi wa tuzo ya Afrika katika masuala ya uchumi.

Makamo mwenyekiti wa kamati ya tuzo ya ukombozi Afrika, Mwebesa Rwebugia ameieleza BBC kwamba rais Magufuli ameibuka mshindi kutokana na mchango wake wa kiuchumi hasaa katika ukuaji wa miundo mbinu.

Hii ni mara ya pili kwa kiongozi wa Tanzania kupata tuzo hii, baada ya Mwalimu Julius Nyerere kutuzwa pia kutokana na mchango wake wa kuleta uhuru katika nchi za Afrika.

Mwebesa Rwebugia ameeleza kuwa, katika kuegemea kwenye muktadha wa uchumi, kamati iliangalia umaskini ambao unatajwa kuwa adui mkubwa anayefahamika, lakini pia maradhi na ujinga.

Kwa mujibu wa kamati hiyo ya Tuzo ya Ukombozi wa Afrika, ukombozi katika kipengelee cha elimu huangazia elimu na ujinga kama sehemu ya ukombozi.

Tanzania imetolewa mfano wa elimu ya bila malipo kutoka kutoka shule za msingi mpaka sekondari.

Katika suala la umaskini, kamati imeangalizia hatua ya kuwajali watu wa kipato cha chini, ukitolewa mfano wa kusajiliwa kwa 'machinga' katika kuwatambua rasmi kwa shughuli zao, na pia kuondolewa kodi za mazao kwa wananchi.

Lakini sio kila mtu amepokea vyema ushindi huu wa rais Magufuli kutokana na kwamba kiongozi huyo hajakamilisha hata miaka mitano tangu aingie madarakani.
Na Geofrey Odero.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
RAIS MAGUFULI AMEIBUKA MSHINDI WA TUZO YA UKOMBOZI WA AFRIKA RAIS MAGUFULI AMEIBUKA MSHINDI WA TUZO YA UKOMBOZI WA AFRIKA Reviewed by By News Reporter on 7/17/2018 05:50:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.