Loading...

RAIS MAGUFULI ATEUA MKURUGENZI MPYA NSSF

Loading...
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Prof. Godius Kahyarara kuanzia leo tarehe 14 Julai, 2018.

Prof. Kahyarara atapangiwa kazi nyingine.

Kufuatia hatua hiyo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. William Erio kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Erio alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pension wa PPF.

Uteuzi wa Bw. Erio unaanza leo tarehe 14 Julai, 2018.
Na Catherine Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
RAIS MAGUFULI ATEUA MKURUGENZI MPYA NSSF RAIS MAGUFULI ATEUA MKURUGENZI MPYA NSSF Reviewed by By News Reporter on 7/14/2018 03:24:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.