Loading...

JAMAA AMUUA MKEWE NA KUMZIKA SHIMONI - KENYA

Loading...
Maafisa wa polisi katika kaunti ya Bungoma wanamsaka jamaa mmoja aliyemuua mkewe kabla ya kumzika kwenye shimo dogo alilokuwa amechimba.

Tukio hilo lilifanyika katika kijiji cha Sudi tarafa ya Bukembe eneo bunge la Kanduyi siku ya Alhamisi, Julai 12. 

Kwa mujibu wa ripoti tulizozipata na mtandao wa TUKO.co.ke, Gerald Nyongesa aliyemuua mkewe na ambaye kabla ya kisa hicho alikuwa ametoka jela baada kuhudumu kifungo chake alitoroka.

Pia, mkewe Gerald aliyemuua alikuwa mlevi kupindukia kila asubuhi akiwa mlevi kwa kunywa chang'aa. 

Polisi wa Nzoia walifika eneo la kisa hicho siku ya Ijumaa, Julai 13 na kuufukua mwili wa Elizabeth Machuma, mwenye umri wa miaka 33, na mama wa watoto wawili na kuupeleka katika monchwari ya Hospitali ya Rufaa ya Bungoma.

Naibu chifu wa Bukembe Mashariki, Martin Kwata alisema kuwa maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi na msako katika kumsaka mshukiwa.
Paskali Joseph.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
JAMAA AMUUA MKEWE NA KUMZIKA SHIMONI - KENYA JAMAA AMUUA MKEWE NA KUMZIKA SHIMONI - KENYA Reviewed by By News Reporter on 7/14/2018 03:11:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.