Loading...

RAIS MAGUFULI KUHUDHURIA UTIAJI SAINI DARAJA LA SELANDER LEO

Loading...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Mhe. Lee Nak-yeon leo tarehe 23 Julai, 2018 watashuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa daraja jipya la Selander Jijini Dar es Salaam na njia zake.

Hafla ya utiaji saini wa mkataba huo itafanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) itatiliana saini na mkandarasi eneo aliyeshinda zabuni ya ujenzi wa daraja hilo.

Daraja la Selander litaunganisha eneo la Agha Khan katika barabara ya Barack Obama na eneo la Coco Beach katika makutano ya barabara za Kenyarra na Toure.

Katika tukio jingine, Mhe. Rais Magufuli atapokea gawio la kipindi cha mwaka 2017/18 kutoka Wakala, Kampuni, Taasisi na Mashirika ya Umma 47 ambayo Serikali inamiliki hisa.

Hafla ya kupokea gawio itafanyika katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Matukio haya yatarushwa moja kwa moja na vituo vya redio, televisheni na mtandao kupitia www.ikulu.go.tz kuanzia saa 3.30 asubuhi.
Na Geofrey Okechi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
RAIS MAGUFULI KUHUDHURIA UTIAJI SAINI DARAJA LA SELANDER LEO RAIS MAGUFULI KUHUDHURIA UTIAJI SAINI DARAJA LA SELANDER LEO Reviewed by By News Reporter on 7/23/2018 08:46:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.