Loading...

JINSI KAMARI YA MPIRA ILIVYOMTUMBUKIZA JAMAA KATIKA JANGA LA UMASIKINI

Loading...
Jamaa mmoja raia wa Kenya alieleza jinsi alivyoingia katika deni kubwa kutokana na kuwa teja wa kamari. Mkenya huyo ambaye jina lake lilihifadhiwa alikuwa amechoka kuisha maisha ya ukabwela.

Siku moja akiwa ofisini kwake, alisikia mwenzake amebahatika na kushinda pesa za Kikenya Sh130,000 kwa kucheza kamari ya mpira baada ya kutabiri shindano la kandanda.

Alikuwa na sh500 tu mfukoni kwa siku hiyo. Usiku ulipofika, aliamua kujiunga na mchezo wa kamari kwa kutumia simu yake kwa lengo la kujinufaisha.

Aliweka pesa hizo kama 'BET' huku akitumainia kuwa angeshinda lakini hakubahatika kushinda. Siku iliyofuatia, alikopa kiasi cha pesa kutoka M-Shwari aende kazini. Lakini pia hakukata tamaa na aliendelea kukopa kidigitali.

Mwishoni mwa mwezi, alicheza kamari mshahara wote wa pesa Kikenya Ksh17,000 na hakupata chochote. Alijitahidi kulipiza kisasi licha ya kuwa alikuwa amekopa pesa nyingi kutoka kwa apu kadhaa za simu na wala hakubahatika chochote.

Alianza kuchukua mikopo kutoka kwa apu karibia zote, Tala, Branch, na zingine nyingi akiwa na matumaini ya kushinda lakini wapi! Alizoshinda zilikuwa kidogo kuliko alizotumia.

Alipata mikopo kutoka apu zaidi ili kugharamia mahitaji yake na kucheza kamari. Simu yake kwa sasa imejaa apu za kukopa pesa na zote zinadai kurejeshewa pesa zao.

Kufikia sasa ana mikopo ya KSh 633,540 huku akihofia kuorodheshwa kwa CRB na labda kukamatwa kwa sababu ya pesa alizokopa kutoka kwa marafiki.

Kisa na maana cha hadithi, ondoka uchezaji kamari au utakumaliza. Hauwezi kukusaidia kuwa tajiri! 

Kisa hiki kilichapishwa mara ya kwanza katika jukwaa la ProjectSensitize.
Na Neema Joshua.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
JINSI KAMARI YA MPIRA ILIVYOMTUMBUKIZA JAMAA KATIKA JANGA LA UMASIKINI JINSI KAMARI YA MPIRA ILIVYOMTUMBUKIZA JAMAA KATIKA JANGA LA UMASIKINI Reviewed by By News Reporter on 7/21/2018 07:26:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.