Loading...

WATU ZAIDI YA 1,000 WAFUTIWA PASSPORT NCHINI UGANDA

Loading...
Zaidi ya watu 1,000 huko Masaka, Mukono, Wakiso, Bukomansimbi na wilayani Lyantonde wamehatarisha pasi zao kufutwa kufuatia ripoti iliyosema kuwa walitumia nyaraka za kugushi kutengeneza pasi hizo.

Hii ilibainika baada ya kukamatwa maafisi huamiaji wawili waliokuwa wakifanya kazi Masaka siku ya Alhamisi ambao waliripotiwa kuwasaidia watu hao pasi hizo.

Kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa wilaya ya Masaka, Bw Joseph Sekasamba ambaye aliagiza kukamatwa kwa afisa hao wawili mara moja, mshukiwa wa kwanza ni mwanamke na mwingine mwanaume.

Washukiwa walihusika na kugushi mihuri ya ofisi za uhamiaji huko Masaka.

Mpaka sasa washukiwa hao wametupiliwa rumande ili wafikishwa mahakamani kwa ajili ya hukumu yao.
Na Geofrey Okechi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WATU ZAIDI YA 1,000 WAFUTIWA PASSPORT NCHINI UGANDA WATU ZAIDI YA 1,000 WAFUTIWA PASSPORT NCHINI UGANDA Reviewed by By News Reporter on 7/21/2018 06:32:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.