Loading...

RAIS WA CAMEROON PAUL BIYA KUWANIA MUHULA WA 7 MWEZI OKTOBA

Loading...
Rais wa Cameroon Paul Biya, ambaye yuko madarakani kwa karibu miaka 36 sasa, ametangaza Ijumaa wiki hii kuwa atawania muhula wa saba katika uchaguzi wa urais wa Oktoba 7.

Rais Biya ana umri wa miaka 85 na muhula wa rais ni wa miaka saba nchini Cameroon.

"Wananchi wenzangu wa Cameroon na wale waishio nchi za kigeni, tunajua changamoto ambazo tunakabiliana nazo kwa Cameroon, yenye umoja, usalama na amani, nakubali kuitikia malalamiko yenu ya haraka, nitakuwa mgombea urais katika uchaguzi ujao wa urais" Paul Biya ameandika kwenye ukurasa wake waTwitter.

Cameroon inaendelea kushuhudia machafuko kutokana na makabiliano ya wanaharakati wanaotaka kujitenga kwa maeneo yao yenye watu wengi wanaozungumza Kiingereza na vikosi vya usalama. Machafuko hayo yameua askari 84 tangu mwezi Septemba mwaka jana kusini magharibi mwa nchi.

Wakazi kutoka maeneo hayo wanapinga kwa mwaka mmoja sasa dhidi ya kile wanachosema kutengwa na kunyanyaswa na serikali ya rais Biya, ambayo ina wajumbe wengi kutoka maeneo kunakozungumzwa Kifaransa.
Na Hamisi Fakhi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
RAIS WA CAMEROON PAUL BIYA KUWANIA MUHULA WA 7 MWEZI OKTOBA RAIS WA CAMEROON PAUL BIYA KUWANIA MUHULA WA 7 MWEZI OKTOBA Reviewed by By News Reporter on 7/14/2018 04:21:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.