Loading...

TANZIA: MBUNGE WA KOROGWE VIJIJINI, STEPHEN HILARY NGONYANI (Prof. MAJI MAREFU) AFARIKI DUNIA

Loading...
Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM) Mh Stephen Hilary Ngonyani (Profesa Maji marefu) afariki dunia. Amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili umethibitisha.

Ikumbukwe Stephen Ngonyani maarufu 'Profesa Majimarefu’ Jumatano Juni 6, 2018 alifiwa na mkewe, Mariam aliyekuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Juni 20 mwaka huu, Ngonyani alisafirishwa kwa ndege kutoka mkoani Dodoma kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa afya yake.

Majimarefu alihamishiwa Muhimbili baada ya kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa siku tatu.

Murugenzi msaidizi wa huduma kwa wabunge, Mvunye Suleiman alisema mbunge huyo anapelekwa MNH kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

Hata hivyo, ugonjwa uliokuwa unamsumbua mbunge huyo haukuwekwa wazi zaidi ya kuelezwa kuwa ana uchomvu kutokana na kufiwa na mkewe.

Amekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini tangu 2010.

Stephen Hilary Ngonyani alizaliwa tarehe 25 Mei 1956.

MSIBA WA 'MAJIMAREFU'; BUNGE KURATIBU MAZISHI.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ametuma salamu za rambirambi kwa familia, wananchi wa jimbo la Korogwe vijijini, wabunge na watanzania kwa wananchi ujumla kufuatia kifo cha mbunge Stephen Hillary Ngonyani maarufu kama Maji Marefu.

Maji Marefu amefariki usiku wa tarehe 2 Julai kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Spika Ndugai, ofisi ya Bunge itashirikiana na familia ya marehemu Maji Marefu ili kuratibu mazishi yake.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
TANZIA: MBUNGE WA KOROGWE VIJIJINI, STEPHEN HILARY NGONYANI (Prof. MAJI MAREFU) AFARIKI DUNIA TANZIA: MBUNGE WA KOROGWE VIJIJINI, STEPHEN HILARY NGONYANI (Prof. MAJI MAREFU) AFARIKI DUNIA Reviewed by By News Reporter on 7/03/2018 07:22:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.