Loading...
WATEJA 60 waliofanya malipo katika nyumba za maendeleo zinazojengwa na mradi wa Fumba Town, wamekabidhiwa nyumba zao.
Mkurugenzi Mkuu wa mradi huo, Sebastian Diezold, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika sherehe ya kuwakabidhi wateja nyumba hizo, zilizofanyika Fumba.
Alisema mradi umeweka aina 17 za majengo yatakayokuwa na makaazi 980 ambapo hatua hiyo ni miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana kwani imewarahisishia wananchi kupata makaazi bora.
Alisema mradi umelenga kuweka viwango bora vya makaazi na huduma bora za kijamii kwa kila mwananchi atakaeishi ndani ya mji huo.
Hata hivyo, alisema nyumba hizo zipo zilizojengwa kwa kutumia utaalamu wa PREFAB ambao unatumia mchanga kidogo, mbao na mawe hali ambayo imesaidia kukabiliana na uharibifu wa mazingira.
Mbali ba hayo, alisema katika mji huo kuna huduma zote muhimu ikiwemo maeneo ya mapumziko, biashara, michezo na ibada.
Alisema serikali inaweka mkazo wa kuwa na makaazi salama katika mipango yake kwa wananchi wake na kuwapa hamasa ya kuendelea kushirikiana na wadau wengine katika sekta ya ujenzi pamoja na kujibidiisha kufanikisha mradi huo.
“Kwa namna ya pekee napenda kuwashukuru viongozi wa serikali hasa Rais wa Zanzibar kwa ushirikiano anaotupa,” alisema.
Alisema katika ujenzi huo wanapata ushirikiano kutoka kundi la kampuni na taasisi kwa lengo la kutekeleza mradi huo kwa ufanisi na kwa wakati.
Mji wa maendeleo wa Fumba ni moja ya miradi mikubwa ya ujenzi wa mji ya kisasa Zanzibar unaotekelezwa na kampuni ya CPS ambao ulianza mwanzoni mwa 2016 na lengo ni kujenga nyumba 3,000.
Na Hamisi Fakhi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

WALIMALIZA MALIPO WAKABIDHIWA NYUMBA FUMBA
Reviewed by By News Reporter
on
7/04/2018 11:57:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: