Loading...

WANAHARAKATI WAPAMBANA NA MIGOGORO YA NDOA

Loading...
WANAHARAKATI wa kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia Mkoa wa Kaskazini Unguja wameishauri elimu ya ndoa itolewe kwa masheikh na mawalii wanaoozesha ili kuepuka utata wa ndoa.

Wakizungumza katika kikao kilichowashirikisha wanaharakati hao na wajumbe kutoka Chama cha Waandishi Wahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), katika skuli ya Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja, walisema kutokuwa na elimu ya kutosha juu masuala hayo yanachangia kutokuwepo maelewano baina ya wanandoa.

Walisema kuna tabia kwa baadhi ya wazazi kuwaozesha watoto kwa ndoa za kukamatiwa bila ya kufuata misingi ya dini na taratibu za ndoa.

Jecha Makame, alisema hali hiyo inasababisha kutokea migogoro, kuongezeka talaka na kusababisha kuongezeka kwa vitendo vya udhalilishaji.

Aidha alisema ni vyema serikali kuliangalia kwa kina suala hilo kwani lina umuhimu mkubwa kwa jamii katika kupunguza masuala hayo.

Wakizungumza udhalilishaji, walisema kesi nyingi huishia polisi na kutolewa suluhu kutokana na wahusika kuoneana muhali bila ya kujali athari zinazompata aliyefanyiwa vitendo hivyo.

Ashura Ali mjumbe kutoka JUWAMAKU, aliwasihi wazazi na walezi kuwa na tabia ya kufuatilia watoto wao na kuwajengea mikakati imara katika makuzi yao ili waweze kujitambua na kujikinga na vitendo vya udhalilishaji.

Aidha alitumia fursa hiyo kuiomba jamii kurejesha malezi ya zamani na kufuata mila, silka na tamaduni za kizanzibari ili kupunguza vitendo hivyo.
Na Mohamedi Makame.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WANAHARAKATI WAPAMBANA NA MIGOGORO YA NDOA WANAHARAKATI WAPAMBANA NA MIGOGORO YA NDOA Reviewed by By News Reporter on 7/04/2018 10:29:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.