Loading...
Mwandishi mwanamke kutoka Kenya ameshinda tuzo maarufu ya uandishi Afrika, tuzo ya Caine inayowatunuku waandishi bora kutoka Afrika.
Makena Onjerika ameambia mtandao wa habari wa BBC kwamba atatoa nusu ya zawadi ya tuzo hiyo ya £10,000 ($13,000) kwa hisani kusaidia shughuli za kuwasaidia na kuwaokoa watoto wa kurandaranda mitaani.
"Kwa pesa zilizosalia nitanunua gari na pengine pikipiki ya kunisaidia kukwepa foleni Nairobi," amesema.
Hadithi yake ambaye imemshindia tuzo hiyo ni kuhusu kisa cha mtoto wa mtaani Kenya anayeitwa Meri.
Majaji wamemsifu kwa kukosa kuathiriwa na hisia za moyoni na ukatili wa utani wake.
Onjerika anasema ameshangazwa na ushindi huo na kusema alikuwa anatarajia kwamba hangeshinda tuzo hiyo ambayo hutolea kila mwaka kwa mwandishi Mwafrika kwa hadithi fupi iliyochapishwa kwa lugha ya Kiingereza.
Hadithi yake yenye kichwa Fanta Blackcurrant ilishinda kutoka kwa orodha ya mwisho ya hadithi tano.
Onjerika, ambaye amehitimu uandishi kutoka kwa mpango wa uandishi wa ubunifu wa MFA Creative Writing katika Chuo Kikuu cha New York anasema aliamua kuandika kuhusu watoto wa mtaani kwani "Kenya - mimi nikiwepo - huwa haiwatazami watoto wa mtaani kama watoto.
"Huwa kuna watoto, na kisha kuna 'chokora'," anasema.
Watoto wanaoangaziwa katika Fanta Blackcurrant hufanikiwa kujikimu kimaisha Nairobi kutokana na ujuzi wao wa kiasiri na kujitolea kwao.
Moja ya ndoto za Meri ni kupata soda kubwa aina ya Fanta Blackcurrant ambayo atakuwa akiinywa kila siku na isiishe.
Baada ya kupata kipaji cha kuwaibia wanawake wafanyabiashara waliofanikiwa, anapigwa sana na wahalifu wengine lakini anafanikiwa kunusurika na kuuvuka mto, na hadithi inaishia kwa maneno "kutoka hapo hatujui alikwenda wapi."
Tofauti na watoto wengine katika hadithi hiyo ambao wanapigania sana kukubalika katika jamii, Onjerika ameambia BBC kwamba mhusika huyo mkuu katika Fanta Blackcurrant zaidi anataka kujivunia utamu wa maisha.
Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

MWANDISHI WA KENYA KUTOA MAMILIONI YA PESA, KWA WATOTO WA MITAANI
Reviewed by By News Reporter
on
7/04/2018 09:17:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: