Loading...
Hayo yamesemwa jana na waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu, alipoifanya ziara katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam kukagua miundombinu na huduma za afya.
Amesema malengo makuu ya wizara katika kusimamia hospitali hizo ni kuhakikisha uwepo wa madaktari bingwa na kuboresha miundombinu ya huduma za dharura, afya ya mama na mtoto na huduma za wagonjwa mahututi. Maamuzi hayo yanakuja miezi kadhaa tangu agizo la Rais John Magufuli kuitaka wizara hiyo kuzisimamia hospitali hizo badala ya TAMISEMI iliyokuwa ikizisimamia hapo awali.
Na Salma Omari.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
HOSPITALI ZA MIKOA, RUFAA SASA MIKONONI MWA MHE. UMMY MWALIMU
Reviewed by By News Reporter
on
7/03/2018 12:34:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: