Loading...

MWANAMKE 'ALIYEKUFA' AFUFUKIA MOCHWARI

Loading...
Mwanamke mmoja nchini Afrika Kusini amezua taharuki baada ya kupatikana akiwa hai katika jokofu la kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.

Mwanamke huyo alifikishwa katika chumba hicho baada ya madaktari kusema alikuwa amefariki dunia kufuatia ajali ya barabarani.

Katika uchunguzi wao madaktari walisema hakuonyesha dalili zozote za kuwa hai na hivyo kutamka kuwa alikuwa amepoteza maisha.

Mafundi wanaofanya kazi katika chumba hicho ndio waliogundua kuwa mwanamke huyo alikuwa hai na hatimaye kumwondoa.

Aliletwa kwenye chumba hicho akidhaniwa amepoteza maisha yeye na wenzake wawili baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka na kuvingirika zaidi ya mara tatu.  Wawili hao waliobakia ndiyo waliofariki dunia.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AFP, mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina lake sasa amekuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Leratong iliyoko Magharibi mwa mji wa Johannesburg.

Familia ya mwanamke huyo aliyegunduliwa kuwa hai imesema wamepata mshtuko na wana wasiwasi mkubwa kuhusu mkasa huo.
Na Jane Mkeu.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MWANAMKE 'ALIYEKUFA' AFUFUKIA MOCHWARI MWANAMKE 'ALIYEKUFA' AFUFUKIA MOCHWARI Reviewed by By News Reporter on 7/03/2018 11:23:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.