Loading...

WAZIRI UMMY AANDIKA HISTORIA KIJIJI CHA MWAMGONGO KIGOMA

Loading...
Kutokana na vifo vya wanawake wajawazito na watoto kushamiri Wizara ya Afya na Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Kupitia Waziri Ummy Ally Mwalimu, Amesema serikali imetenga kiasi cha shs.milioni 400 ili kukabiliana na tatizo hilo.

Waziri Ummy aliyesema hayo Jana julai 20 akiwa katika ziara yake huko Mkoani Kigoma Ambapo alitembelea Kijiji cha Mwamgongo na kuacha historia ya kuwa kiongozi wa Pili kutembelea kijiji hicho Tangu Baba wa Taifa Mwl Nyerere alipofanya ziara mwaka 1968.
” Mwaka 2017/18 serikali imepeleka sh.milioni 400 kwa ajili ya kuboresha Kituo cha Afya cha Mwamgongo ili kukiwezesha Kutoa Huduma kamili za uzazi wa dharura ikiwemo upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni (CEMONC) ili kupunguza Vifo vya wajawazito na watoto.”Alisema Waziri Mwalimu.

Pia Waziri Wa Afya alisema Pesa hizo zitatumika kujenga Chumba cha Upasuaji (Theatre) Wodi ya Wazazi, Maabara na Nyumba ya Mtumishi.

Aidha Kutokana na vilio vya wananchi wa kijiji hicho Mhe.Ummy Amesema wizara yake imejipanga kununua boti tatu (3) za mwendokasi zitakazosaidia kubeba wagonjwa wanaohitaji rufaa hasa wanawake wajawazito katika maeneo yanayozungukwa na Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria na Visiwa vya Mafia.
Na Hamisi Fakhi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WAZIRI UMMY AANDIKA HISTORIA KIJIJI CHA MWAMGONGO KIGOMA WAZIRI UMMY AANDIKA HISTORIA KIJIJI CHA MWAMGONGO KIGOMA Reviewed by By News Reporter on 7/21/2018 05:45:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.