Loading...
Wakimbizi kutoka nchini Burundi zaidi ta elfu 24 waliokuwa wamekimbilia nchini Tanzania wamerejea nchini mwao tangu mwanzoni mwa Januari mwaka 2018.
Tanzania ndio taifa pekee Afrika Mshariki ambalo limepokea idadi kubwa ya wakimbizi kutoka Burundi tangu kuzuka kwa ghasia mwaka 2015.
Tangu Januari mwaka 2018 , wakimbizi zaidi ya elfu 24 kutoka Burundi waliokuwa katika kambi za wakimbizi nchini Tanzania wamerejea nchini Burundi.
Kulingana na taarifa zilizotolewa na wizara ya mambo ya ndani nchini Burundi na usimamizi wa Terence Ntahiraja ni kwamba watu 24,223 wamekwishapokelewa nchini Burundi wakitokea nchini Tanzania.
Wakimbizi kutoka Burundi ambao wamechukuwa uamuzi wa kurejea katika taifa lao, wamechukuwa uamuzi huo kwa hiari yao baada ya kupokea taarifa kwa amani imekwisharejea kote nchini humo.
Baadhi ya wakimbizi wamefahamisha kuwa hali ngumu katika kambi za wakimbizi kama uhaba wa chakula ni moja miongoni mwa sababu zilizowapelekea kuchukua uamuzi huo.
Kwa upande mwingine katika ziara yake nchini Rwanda , kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa Filippo Grandi alifahamisha kuwa rais wa Rwanda ilikubaliana nae kuhusu mazungumzo kwa lengo la wakimbizi kutoka Burundi walioko nchini Rwanda na uwezekano wa kurejea katika taifa lao.
Na Hamisi Fakhi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

ZAIDI YA WAKIMBIZI ELFU 24 KUTOKA TANZANIA WAREJEA NCHINI BURUNDI
Reviewed by By News Reporter
on
7/23/2018 09:01:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: