Loading...
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amezungumzia kujiuzulu kwa mbunge wa Monduli, Julius Kalanga akiwataka wananchi wasife moyo.
“Nimesikia taarifa za kujiuzulu kwa mbunge wangu wa Monduli, Julius Kalanga. Kwa sababu zozote zile atakazokuwa amezitoa, hiyo ni haki yake kikatiba,” amesema Lowassa katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake leo Julai 31, 2018.
Lowassa aliyewahi kuwa mbunge wa Monduli kupitia CCM na waziri mkuu kuanzia mwaka 2005 hadi 2008 amesema, “Najua wana Monduli wote nikiwemo mimi uamuzi huo umetuhuzunisha na kutuumiza, lakini nawaomba msife moyo hata dakika moja zaidi kitendo hicho cha Kalanga kizidi kutupa nguvu, ari, hamasa na mori zaidi wa kuendeleza mapambano ya kuitafuta demokrasia na mabadiliko ya kweli.”
Amesema, “Hakuna jipya katika hili, ni kawaida kwa wana siasa duniani kuhama vyama vyao na kubadilishana vijiti.”
“Moto ule tuliouwasha 2015 hauwezi hata mara moja kuzimwa na mbinu hizi.
Wataondoka kina Kalanga wengi tu lakini kasi ya moto ule jinsi ilivyo sasa ndani ya mioyo ya Watanzania ni ya moto wa kiangazi.”
Mwanasiasa huyo amesema, “Monduli imetupa heshima kwenye harakati za mabadiliko, naomba msife moyo.”
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

ALICHOSEMA LOWASSA KUJIUZULU MBUNGE WA MONDULI
Reviewed by By News Reporter
on
8/01/2018 09:23:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: