Loading...

BOBI WINE KAMATWA NA POLISI BAADA NA KUKUTWA NA SILAHA ZA MOTO

Loading...
Mbunge wa jimbo la Kyaddondo Mashariki, Mh. Robert Kyagulanyi aka Bobi Wine ambaye alikamatwa siku ya Jumatatu katika jiji la Arua akiwa pamoja na wapinzani wenzake wa upinzani, ameshitakiwa mbele ya mahakama kuu iliyopo Gulu kwa makosa ya kumiliki silaha za moto na mafataki kinyume na sheria.

Mahakama iliongozwa na Lt Gen Andrew Gutti.

Kulingana na kauli iliyosemwa siku ya Alhamisi na msemaji wa jeshi la kulinda wananchi, Brigedia, Richard Karemire, Mbunge huyo aliburuzwa rumande hadi Alhamisi ya wiki ijayo.

"Kama sehemu ya uchunguzi katika vitendo hivi vya uvunjifu wa amani, Polisi walimkamata kiongozi mkuu na washiriki wote wakiwemo Mh. Robert Ssentamu Kyagulanyi mbunge wa jimbo la Kyadondo.
Wakati wa msako katika chumba cha hoteli aliyokuwa amefikia walikuta mafataki na risasi ambazo yeye atakiwi kumiliki," mpaka sasa Bobi Wine ameumizwa vibaya na wanajeshi katika jaribio la kumbana ili atoe maelezo kamili jinsi silaha hizo alipo zipata.

Hali yake ya kiafya sio nzuri, na imeperekea mke wake kuomba aonane naye angalau kumfariji lakini bado ameshikiliwa na jeshi la polisi.
Na Hamisi Fakhi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
BOBI WINE KAMATWA NA POLISI BAADA NA KUKUTWA NA SILAHA ZA MOTO BOBI WINE KAMATWA NA POLISI BAADA NA KUKUTWA NA SILAHA ZA MOTO Reviewed by By News Reporter on 8/17/2018 07:31:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.