Loading...

HATIMAYE JOSE MOURINHO ASEMA NENO BAADA YA KIPIGO CHA 3 - 2 NA BRIGHTON

Loading...
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho, amekubali kuwa wachezaji wake walifanya makosa wakti wa mchuano dhidi ya Brighton & Hove Albion ambayo yalifanya timu hiyo kushindwa kwa mara ya kwanza katika msimu.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea alisema hilo alipokuwa akijibu maswali ya wanahabari ambao walimuuliza kilichoendelea uwanjani. 

Mwanahabari mmoja aliuliza, “Man U ni timu iliyo na umaarufu mwingi, ilikuwa sawa ilivyofanya uwanjani?”

Kwa kujibu swali hilo Mourinho alisema, “Tulifanya makosa na tuliadhibiwa na makosa hayo,” na kumpuzilia mbali mwanahabari huyo alipomuuliza kuhusiana na ushirikiano wa wachezaji uwanjani.

Mechi iliyochezwa siku ya Jumapili Man U ilicharazwa 3-2 na Brighton & Hove Albion ingawa ni timu isiyo na ushawishi mkubwa.

Mchuano huo ulikuwa katika uwanja wa Amex, Jumapili Agosti 19. 

Man U ilishinda Leicester City 2-1 katika mchuano wa kufungua msimu katika uwanja wa Old Trafford ambapo Paul Pogba na Luke Shaw waliipa timu hiyo ushindi waliostahili.
Na Fatma Pembe.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
HATIMAYE JOSE MOURINHO ASEMA NENO BAADA YA KIPIGO CHA 3 - 2 NA BRIGHTON HATIMAYE JOSE MOURINHO ASEMA NENO BAADA YA KIPIGO CHA 3 - 2 NA BRIGHTON Reviewed by By News Reporter on 8/21/2018 08:41:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.