Loading...

HISTORIA YETU: FAHARI KUMI NA MOJA ZA ZANZIBAR

Loading...
1. Zanzibar ndiyo nchi pekee duniani iliyopigana vita vya muda mfupi kuliko vyote, ilikuwa vita kati ya Sultan na watawala wa Kiingereza, Agosti 27, 1896. Vita ilidumu kwa dakika 38 hadi 45 Sultan akasalimu amri.

Vita hii ilitokana na kifo cha Sultan Hamad bin Thuwaini, Agosti 25, 1896 uliibuka mvutano nani arithi kiti, akarithi Sultan Khalid bin Barghash.

Inaelezwa sababu ya vita ni Waingereza kupanga nani atamrithi Sultan Thuwain ambaye alikuwa akiwapendelea watawala, Waingereza walitaka Hamud bin Muhammed ndio arithi maana alionekana ana tabia za kizungu.

Baada ya Sultan Khalid kusalimu amri na kukimbilia Tanganyika ambayo wakati huo ilikuwa chini ya utawala wa Kiujerumani, Waingereza walimweka mtu waliyemtaka ambaye ni Sultan Hamud.

2. Katika Afrika na hata maeneo mengine ya dunia Zanzibar ndiyo ya kwanza kuwa na usafiri wa treni ya umeme mwishoni mwa miaka ya 1800, baadaye katika mwaka 1904 ilijenga reli ya treni ya kawaid iliyoitwa Treni ya Bububu kabla ya nchi nyingine za Afrika Mashariki.
Kampuni iliyopewa zabuni ya kujenga treni hiyo n Arnold Cheney and Co.  

3. Zanzibar ndiyo ya kwanza katika nchi zilizoendelea na Afrika nzima kuwa na taa za umeme barabaarani. Ilianza na taa zilizotumia mafuta ya taa mwaka 1870 zilizowekwa barabarani baadaye zilikaja taa za umeme, zilipita katika maeneo ya bandarini hadi Mbweni, inatajwa ilitokana na athari za treni ya umeme iliyoanza miaka ya nyuma.
Itakumbukwa Jiji la London, Uingereza lilianza kuweka taa za barabarani mwaka 1889, miaka 19 baada ya Zanzibar kuweka taa barabarani.  

4. Jumba la maajabu lililojengwa mwaka 1883 na Sultan Baraghash bin Said lilikuwa na mambo mengi ya starehe kuliko majengo mengi katika miaka hiyo, hata Ulaya hakukuwa na majumba aina yake. 

Miongoni mwa vitu vya maajabu vilivyokuwemo ni lifti iliyotumia umeme, ambapo ni jengo la kwanza katika ukanda huu wa Afrika Mashariki kuwa na lifti. Hadi sasa kuna baadhi ya vitu vipo ndani ya jengo hilo hakuna jengo lingine lolote lililowahi kuviweka.

5. Zanzibar pia ni miongoni mwa sehemu ya kwanza duniani kuwa na Dispensary, ilijengwa mwaka 1887 na tajiri wa Kiismailia, Tharia Topan kufurahia miaka 50 ya Malkia Victoria wa Uingereza. Jengo hili hadi sasa lipo Barabara ya Mizingani, ni miongoni mwa majengo yanayotazama Bahari ya Hindi.

Fahamu kuwa Dispensary ya kwanza duniani ilijengwa mwaka 1861 ikiitwa Straford and South Essex Dispensary, ilifunguliwa Julai 1861 na Dk. William Elliot. 

6. Zanzibar ni miongoni mwa nchi za mwanzo kuwa na bwawa la ndani la kuogelea matajiri, lenye maji ya moto na sehemu za kupumzika. Eneo hili linaitwa Hamamni Persian Baths, lilijengwa mwaka 1870 kwa ajili ya Sultan Barghash bin Said kuogelea na kupumzika na matajiri wa mjini. Bwawa hili lilikuwa na vyoo na mabafu ya kisasa, sehemu ya kunyoa nywele na mikahawa kwa ajili ya vinywaji na vyakula.

Mabwawa ya kuogelea yana historia ndefu miaka mingi kabla ya kuzaliwa Kristo, lakini ya aina hii yalianza kujengwa mwaka 1844 jijini London. Miaka 26 baadaye Zanzibar wakajenga pia.

7. Katika kitabu kilichoandikwa katika karne ya kwanza hadi ya tatu ‘Periplus of the Erythrean Sea’ kinabainisha kuwa Zanzibar ni miongoni mwa miji ya kwanza kuwa na maendeleo katika dunia. Waarabu, wahindi na wangazija walitumia visiwa vya Unguja ambavyo katika kitabu hicho wameita kama Menuthias, kwa ajili ya kupumzika au kwa ajili ya likizo (Holidays). Ndipo walipopata wazo la kuanzisha biashara katika ukanda Pwani ya Afrika Mashariki. Tafsiri yake wageni katika ukanda huu walinza kufika Zanzibar kwanza ndipo wakasambaa.

8. Zanzibar pia ndiyo eneo la kwanza katika ncha Kusini mwa Jangwa la Sahara kuwa na majumba marefu kwa ajili ya makazi ya watu. Majengo ya Michenzani yaliyojengwa katika serikali ya awamu ya kwanza chini ya Rais Abeid Amani Karume kwa msaada wa Ujerumani Mashariki katiika miaka ya mwishoni mwa 1960.

9. Zanizbar ndiyo nchi ya kwanza katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati pamoja na kusini mwa jwangwa la Sahara kuwa na kituo cha televisheni ya rangi mwaka 1973.

10. Zanzibar ndiyo nchi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Jangwa la Sahara nay a pili kwa Afrika baada ya Misri kuwa na mwanamuziki aliyerekodi nyimbo zake katika Santuri. Sitti binti Saad. Alirekodi sauti yake mwaka 1928 nchini India katika kampuni ya Columbia Records and His Master’s Voice.

Itakumbukwa bibi huyu aliyezaliwa mwaka 1880 katika Kijiji cha Fumba alianza kuimba kama masihara, ndipo akasikika na wakubwa. Mwaka huo 1928 akasikika na kampuni za Columbia Records wakamuita nchini India ambako pia alikutana na muimbaji mashuhuri wa Misri, bibi Umu Kulthum naye akirekodi, manake walikuwa wanawake wa kwanza wa kiafrika kurekodi katika studio hiyo katika miaka hiyo ya kiza jijini Mumbai, India.

Kampuni ilianza kwa majaribio kurekodi sauti ya Sitti bint Saady, lakini katika hali ya kushangaa waliuza kopi 900 ndani ya miaka miwili ya mwanzo, hadi kufika mwaka 1931 miaka minne tangu waingie naye mkataba waliuza kopi 72,000.

Kutokana na mshangao huo na mahitaji makubwa ya sauti ya bibi huyu, watu wengi walijazana Zanzibar kumsikiliza akiimba mubashara majukwaani pale Ngome Kongwe, ndipo Columbia Records wakaona wanachelewa, wakajenga studio hapohapo Zanzibar maana waliona kumsafirisha hadi India ni kumchelewesha, kwa hiyo hili la Zanzbar kuwa na studio ya kwanza katika ukanda huu nimewapa bure, maana lilitakiwa kuwa jambo la 11.
Na Paskali Joseph.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
HISTORIA YETU: FAHARI KUMI NA MOJA ZA ZANZIBAR HISTORIA YETU: FAHARI KUMI NA MOJA ZA ZANZIBAR Reviewed by By News Reporter on 8/21/2018 09:26:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.