Loading...

JINSI TEKNOLOJIA MPYA ITAKAVYOWAPA FURSA YA KUFANYA BIASHARA YA TAXI

Loading...
Mji mkuu wa Korea Kusini umepata madereva wa kwanza wa teksi viziwi wiki hii, kwa msaada wa teknolojia ambayo imezinduliwa ya kupunguza unyanyapaa wa kuwaajiri watu walio na ulemavu huo.

Kulingana na mtandao wa habari wa Korean Times, dereva wawili viziwi walianza kusafirisha abiria kwenye mji mkuu wiki hii wakisaidiwa na teknolojia iliyoundwa na kampuni mpya ya Coactus.

Akielezea jinsi teknolojia hiyo inafanya kazi mtandao wa Yonhap unasema kuwa vifaa hivyo vimewekwa viti vya mbele na nyuma ya teksi na vimeunganishwa na kampuni za teksi za Goyohan au silent Taxi.
Teknolojia hiyo inawezesha mawasiliano ya sauti na ujumbe ulioandikwa kuwasaidia abiria kuelezea maeneo wanataka kwenda na mifumo ambayo wangependa kutumia kulipa.

Iliundwa na kundi la wanafunzi mjini humo na kuongozwa na mwanafunzi aliyefuzu na taalumaa ya uandisi Song Min-pyo.

"Tulitaka kuwapa watu viziwi ajira zaidi," Bw Song aliliambia gazeti la Korea Times.

"Tulijua kuwa wakorea watatoka nje ya gari ikiwa dereva ataanza kuwasiliana akitumia simu na kalamu kwa hivyo tukaunda teknolojia hii.'

Yonhap anasema kuwa Coactus itapunguza unyanyapaa unaowakumba madereva visiwi nchini Korea Kusini.

Watu 255,000 wana matatizo ya kusikia nchini Korea Kusini kwa mujibu wa wizara ya afya.
Na Geofrey Okechi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
JINSI TEKNOLOJIA MPYA ITAKAVYOWAPA FURSA YA KUFANYA BIASHARA YA TAXI JINSI TEKNOLOJIA MPYA ITAKAVYOWAPA FURSA YA KUFANYA BIASHARA YA TAXI Reviewed by By News Reporter on 8/19/2018 07:14:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.