Loading...

MUIGIZAJI MAARUFU INDIA 'PYANKA CHOPRA' AVISHWA PETE YA UCHUMBA

Loading...
Mwigizaji wa kike wa Bollywood wa nchini India, Priyanka Chopra, 36, na muimbaji Mmarekani Nick Jonas, 25 wamethibitisha kuvishana pete ya uchumba kwa sherehe ya kitamaduni iliyofanyika leo Jumamosi asubuhi katika nyumba ya muigizaji huyo katika jiji la Mumbai.

Sherehe hiyo ya kitamaduni itafuatiwa na party ya mastaa baadae usiku ambapo Nick atakutana na marafiki na jamaa wa Priyanka.

Wazazi wa Nick Jonas pia wapo India kuhudhuria sherehe ya ndoa ya mtoto wao sambamba na familia ya Chopra.

Chanzo cha karibu na indianexpress.com mapema kiliweka wazi Chopra tayari amekodisha vyumba 200 vya hoteli kwa ajili ya wageni, wengi wanatarajiwa kutoka Marekani. Ranveer Singh, Karan Johar, Manish Malhotra, Sophie Choudry na Raveena Tandon wanatarajiwa kuhudhuria.

Nick and Priyanka wamevishana pete baada ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi kwa kipindi cha miezi 2.
Na Hamisi Fakhi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MUIGIZAJI MAARUFU INDIA 'PYANKA CHOPRA' AVISHWA PETE YA UCHUMBA MUIGIZAJI MAARUFU INDIA 'PYANKA CHOPRA' AVISHWA PETE YA UCHUMBA Reviewed by By News Reporter on 8/18/2018 05:14:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.