Loading...

HURUMA: POLISI MWANAMKE AJITOLEA KUMNYONYESHA MTOTO HOSPITALI

Loading...
Afisa polisi mmoja wa nchini Argentina alifanya vitendo vya kishujaa na upendo pale alipoamua kumnyonyesha mtoto aliyekuwa akionekana kulia na mchafu ambaye aliletwa katika hospitali ambayo alikuwa kama mlinzi.

Celeste Ayala alikuwa anafanya kazi katika hospitali ya watoto ya Sor Maria Ludovica huko Buenos Aires, Argentina wakati mtoto alipofikishwa hospitalini hapo akiwa analia mkiwa.

Afisa huyo alimuomba ruhusa daktari kama angeweza kumnyonyesha mtoto huyo kwa kuwa alimuona akiwa mwenye njaa na wafanyakazi wa hospitali walikuwa wametingwa na kazi, hivyo hawakuwa na muda naye.

Ruhusa ilitolewa na Ayala alimpakata mtoto huyo na kuanza kumnyonyesha, na kunyamaza mara moja.

Rafiki wa afisa huyo, Marcos Heredia, alisema wafanyakazi wa hospitali hiyo walisema mtoto huyo ni 'mchafu', lakini Ayala hakujali. Akaamua kumpiga picha wakati anamnyonyesha mtoto huyo mwenye njaa na kuirusha mtandaoni.

Alidai anataka kuonyesha umma kuwa tunapaswa kuwa na upendo wa namna kama ya Ayala bila kujali hali ya mtu. Picha hiyo ilipata kupendwa na watu 68,000, 94,000 kurushwa sehemu nyingine, kuwa na maoni makini 300.
Na Mary Mkeu.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
HURUMA: POLISI MWANAMKE AJITOLEA KUMNYONYESHA MTOTO HOSPITALI HURUMA: POLISI MWANAMKE AJITOLEA KUMNYONYESHA MTOTO HOSPITALI Reviewed by By News Reporter on 8/18/2018 04:32:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.