Loading...

BREAKING NEWS: ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA 'KOFFI ANNAN' AFARIKI DUNIA

Loading...
Mwanadiplomasia mkuu na aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Koffi Annan ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 80.

Annan ameripotiwa kufariki akiwa nchini Uswizi siku ya Jumamosi,Agosti 18 baada ya kuugua kwa muda mfupi. 

Taarifa za kifo chake kimetangazwa na familia yake.

"Ni huzuni kwa familia ya Annan na Kofi Annan Foundation inatangaza kuwa Kofi Annan, aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Kimataifa na mshindi wa tuzo la amani la Nobel ameaga dunia leo siku ya Jumamosi, Agosti 18," Walisema katika taarifa yao. 

Familia yake ilimsifu kama kiongozi wa kimataifa, mwenye busara aliyepigania ulimwengu wenye amani. Endelea kufuatilia blogu yako pendwa kupata taarifa kamili ya maziko.

'WOTE TUNASEMA PUMZIKA KWA AMANI MAHALI PEMA PEPONI, AMINA'.
Na Peter Godwin.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
BREAKING NEWS: ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA 'KOFFI ANNAN' AFARIKI DUNIA BREAKING NEWS: ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA 'KOFFI ANNAN' AFARIKI DUNIA Reviewed by By News Reporter on 8/18/2018 03:36:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.