Loading...

MAMBO TISA (9) USIYOYAJUA KUMHUSU ARNOLD SCHWARTZENEGGER

Loading...
Wapenzi wa filamu za vita wanamtambua Arnold Schwartzenegger kama mmoja wa waigizaji bora zaidi wa filamu duniani. 

Schwartzenegger alikuwa maarufu sana kwa filamu alizoigiza kama ‘The Terminator’, ‘True Lies’, ‘Total Recall’, ‘Predator’ miongoni mwa filamu zingine nyingi.

Wanawake walipenda sana misuli na umbo la mwili wa Arnold Schwartzenegger, jambo lililowazingua sana mabinti na kwa wakati mmoja ulimteka binti kwa hisia za mahaba mbele ya umma. 

DundiikaNews tunakuletea mambo 9 yakupendeza na kufurahisha kuhusu Arnold (Commando);

1. Jina lake la kati ni Alois na alizaliwa Julai 30, 1947. Ana miaka 71. 

2. Kwa mara ya kwanza, alichukua kifaa cha kujenga misuli akiwa na miaka 13 na akaamua kuifanya taaluma yake akiwa na miaka 14. Alikuwa na bidii sana kwa kiwango cha kuvunja na kuingia kwenye chumba cha mazoezi nyakati za wikendi ambapo kilikuwa kimefungwa akitaka afanye mazoezi. 

3. Wakati wa mafunzo yake ya huduma kwa taifa kwenye jeshi la Australia, alitoroka bila idhini wakati wa mazoezi ya msingi ili ahudhurie mashindano ya kujenga misuli. Alifungwa kwa wiki moja kwenye jela ya kijeshi. 

4. Mwaka 1996, alikuwa wa pili kwenye shindano la ‘Mr. Universe’ na kushindwa na Chester Yorton aliyekuwa mwanamisuli mwenzake.

5. Alijifunza Kiingereza eneo la London East end alipokuwa na mkufunzi wake, Charles Bennett huko Forest Gate. 

6. Alihamia Marekani akiwa na miaka 21 lakini Siskind na Susser, kampuni ya mawakili wa uhamiaji ilidai kuwa alikiuka viza yake na kuwa alikuwa mhamiaji haramu. 

7. Miaka yake ya mwanzo nchini Marekani, alikuwa na uhusiano na Barbara Outland, mwalimu wa Kiingereza.

8. Filamu yake ya kwanza kucheza ilikuwa ‘Hercules’ mwaka wa 1970 jijini New York. Alitumia jina la ‘Arnold Strong’ kwenye filamu hiyo. 

9. Anorld alitengana na mkewe Maria Shriver mwaka wa 2011 baada ya kuwa kwenye ndoa kwa miaka 25. Kutengana huko kulitokea baada yake kufichua kuwa alimzaa mtoto na mwanamke mwingine.
Na Fatma Pembe.





Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MAMBO TISA (9) USIYOYAJUA KUMHUSU ARNOLD SCHWARTZENEGGER MAMBO TISA (9) USIYOYAJUA KUMHUSU ARNOLD SCHWARTZENEGGER Reviewed by By News Reporter on 8/18/2018 02:50:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.