Loading...

VISA NA MIKASA: JAMAA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMBAKA MAMA YAKE

Loading...
Jamaa mmoja kutoka tarafa ya Mugoiri, kaunti ndogo ya Kahuro kaunti ya Murang'a nchini Kenya alifikishwa mahakamani kwa kosa la kumbaka mamayake na kumwambukiza gonjwa hatari la zinaa.

Jamaa huyo kutoka kijiji cha Kandegenye anasemekana kumvamia na kumfanyia mamake mwenye umri wa miaka 63 unyama huo kwani wanaishi katika nyumba moja. 

Polisi walisema kuwa mama huyo aliwaelezea binti zake kuhusu kisa hicho baada ya kupatikana na gonjwa la zinaa.

Akiwa mbele ya hakimu Margaret Wachira katika mahakama Murang'a, jamaa huyo wa miaka 32 aliyakana mashtaka hayo. 

Mahakama iliamuru kuwa jamaa huyo asalie mahabusu hadi pale kesi yake itakapo sikilizwa tena na kuamuliwa.

Kwa mujibu wa SDE, maafisa wa polisi walisema kuwa hayo yalibainika wakati wa kongamano la kifamilia baada ya binti zake mwathiriwa kugundua kuwa mama yao alikuwa akitembea kwa shida sana. 

Walipompeleka hospitalini, ndipo akapatikana na gonjwa la zinaa na kuwaelezea yaliyofanyika.
Na Haika Gabriel.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
VISA NA MIKASA: JAMAA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMBAKA MAMA YAKE VISA NA MIKASA: JAMAA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMBAKA MAMA YAKE Reviewed by By News Reporter on 8/18/2018 02:18:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.