Loading...

MBUNGE AVUA NGUO BUNGENI ILI HOJA YAKE IUNGWE MKONO

Loading...
Mwanasiasa mmoja alizua kizaazaa baada ya kuvua nguo zake wakati wa hotuba katika majengo ya bunge alipokuwa akiwaomba wabunge wenzake kumuunga mkono mwenzao aliyekuwa akiandamwa na serikali kwa madai ya kupanga njama ya kumuua rais.

Mwanasiasa huyo, Gilber Caro mwenye umri wa miaka 43 raia wa Venezuela na mwanachama wa chama pinzani alivua mavazi yake yote alibakia na chupi katika juhudi za kuendelea kumtetea mwenzao wa upinzani, Juan Requesens aliyefungwa jela kwa kuhusishwa kwenye jaribio la kumuua Rais Nicolas Maduro.

Katika hotuba yake, Caro alimsifu Juan, 29, kwa ujasiri wake wa kupigania haki. 

"Naomba umoja katika taasisi hii ili kuitetea jinsi Requesens alivyoenda mitaani kutetea uhuru wa Venenzuela," Alisema.

Mbali na kumtetea Juan, Caro alimshtumu rais Maduro kwa kuwanyima raia haki za kimsingi kama vile chakula na madawa.
Na Neema Bushubo.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MBUNGE AVUA NGUO BUNGENI ILI HOJA YAKE IUNGWE MKONO MBUNGE AVUA NGUO BUNGENI ILI HOJA YAKE IUNGWE MKONO Reviewed by By News Reporter on 8/18/2018 01:47:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.